Monday, September 10, 2012

WAISLAM WAANDAMANA MPAKA WIZARA YA MAMBO YA NDANI!


Waumini wa imani ya dini Kiislamu wakiwa nje ya jengo la wizara ya mambo ya ndani jijini Dar es salaam.

Habari zinasema kwamba kumekuwepo na maandamano katika maeneo ya katikati ya jiji na hatimaye mkusanyiko mkubwa wa waumini wa imani ya dini ya kiislamu nje ya jengo la wizara ya mambo ya ndani lililoko katika mtaa wa Ohio jijini Dar es salaam. 

Habari zaidi zinasema kwamba nia kubwa ya maandamano na mkusanyiko huo ni kuitaka serikali iwaachilie huru waislam wote waliokamatwa na kuwekwa kizuizini kutokana na kugoma kuhesabiwa katika zoezi la Sensa ambalo lilianza mnamo tarehe 26/08/2012 huku likiendelea mpaka hapo tarehe 09/09/2012.

No comments:

Post a Comment