Waziri Shamsi Nahodha
Kupitia safu hii, tumehakikisha tunawaletea siri za ndani kabisa kuhusu kundi la kigaidi la Al-Shabaab.
Kupitia safu hii, tumehakikisha tunawaletea siri za ndani kabisa kuhusu kundi la kigaidi la Al-Shabaab.
Umeshaona jinsi kundi hilo hatari Afrika Mashariki linavyofanya kazi na namna vijana wa Kitanzania wanavyojiunga nalo.
Kubaini yote hayo, uliona jinsi kijana, Aizak Ibnu, 20, alivyosimulia namna yeye na wenzake 24, walivyojiunga na Al-Shabaab lakini 23 walipoteza maisha.
Ipo hatari ya Al-Shabaab kuvamia Tanzania kama ambavyo wamefanya Kenya. Kutokana na tishio hilo, wiki iliyopita, mwandishi wa makala haya, alifanya mahojiano na viongozi wenye mamlaka ya usalama wa nchi.

Waliozungumza ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha na Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba.
Wote walisema kuwa wananchi wawe makini kwa sababu Al-Shabaab hushirikiana na wenyeji kufanikisha uhalifu wao.
WAZIRI NAHODHAWaziri Nahodha alikiri kuwa Al-Shabaab ni hatari, hivyo akawatahadharisha wananchi kuwa makini kwa sababu kundi hilo lina mtandao mpana ndani ya Afrika Mashariki.
“Wananchi wahakikishe wanachukua tahadhari kila sehemu na kutoa taarifa katika vyombo vya dola wakimuona mtu ambaye wana wasiwasi naye.
“Ni vema kuchukua tahadhari mapema na nichukue nafasi hii kuwaomba wananchi kuwa macho kuhusu kikundi hicho. Niwahakikishie kwamba nimewaagiza askari wa idara ya uhamiaji kuhakikisha ulinzi unaimarishwa mipakani.
“Nimewaagiza pia askari polisi kwa kushirikiana na wananchi kupitia polisi jamii, kuhakikisha wanawakamata watu wa mtandao huo popote pale walipo na kuwachukulia hatua za kisheria,” alisema Nahodha.